Wananchi Kalenga wamlalamikia Mbunge kutoonekana jimboni

Na Herieth Rebman | January 11, 2019

Wananchi wa Kata ya Lwamgunge jimbo la Kalenga wamelalamikia kutoonekana kwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Godfrey Mgimwa tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2015, jambo amablo wananchi hao wameeleza kukwamisha shughuli nyingi za maendeleo katika kata hiyo.

Wakizungumza na Country FM wananchi hao wamesema kuwa kuna ahadi nyingi ambazo zimetolewa na mbunge huyo katika kampeni za uchaguzi mkuu mnamo mwaka 2015, lakini tangu achaguliwe kiongozi huyo hajarudi tena kwa wananchi hao kwa utekelezaji kusikiliza kero zao.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi, Alex Malangalila, amekiri kuwepo malalamiko hayo ya wananchi, jambo ambalo amesema linampa ugumu katika utekelezaji wa ilani chama hicho kwa wananchi kutokana na kukosa imani na viongozi wa chama hicho.