Katomali Nchimbi

Presenter

Mzaliwa wa Dodoma na mwenyeji wa Dar, Katomali ni mtangazaji wa vipindi vya burudani na ‘serious” vikiwamo Dira ya Vijana, Top 10, African Swagg na Punch za Home. Anajivunia kuwepo redio Country FM kwasababu ni chombo cha habari kinachofanya kazi kwa weledi na kuwajali wafanyakazi wake. Baada ya kuishi miaka kadhaa nchini Afrika Kusini ambapo amesoma elimu ya sekondari na chuo, Kato anajimudu katika kuzungumza Kizulu.