Chiku Mbilinyi

Station Manager

Chiku ni mbobevu katika masuala ya masoko, utawala na fedha. Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafasi ya kukihuisha kituo kupitia ujuzi wake mkubwa katika kuyatafuta masoko. Amekuwa mwanafamilia wa Country FM kwa takribani muongo mmoja sasa na redio imeyaona matunda makubwa ya juhudi zake katika kuhakikisha kituo kinapiga hatua za mafanikio. Chiku ni mwanamama tegemezi, mpambanaji na mpiganaji asiyekata tamaa kuyafikia malengo yake na wafanyakazi wake.