Mchungaji Msigwa awapa mkakati wabunge Iringa

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewataka wabunge wa Iringa kuungana kupiga kelele ili Serikali ijenge barabara ya lami kutoka Iringa kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Akizungumza leo Alhamisi Februari 14, 2019 katika kikao cha bodi ya barabara mkoani Iringa, Mchungaji Msigwa amesema barabara hiyo ikiwekwa lami itafungua fursa za kiuchumi kwa.

Wananchi Kalenga wamlalamikia Mbunge kutoonekana jimboni

Na Herieth Rebman | January 11, 2019 Wananchi wa Kata ya Lwamgunge jimbo la Kalenga wamelalamikia kutoonekana kwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Godfrey Mgimwa tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2015, jambo amablo wananchi hao wameeleza kukwamisha shughuli nyingi za maendeleo katika kata hiyo. Wakizungumza na Country FM wananchi hao wamesema kuwa.

Iringa yang’ara kwa usafi kitaifa

Na Herieth Rebman | Novemba 23, 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeshika nafasi ya kwanza Kitaifa katika mashindano ya usafi na mazingira nchini. Iringa imetangazwa kushinda Leo katika kilele cha wiki ya usafi na mazingira duniani, sherehe zilizofanyika ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma na mgeni rasmi wa shehere hiyo akiwa Waziri mkuu Wa.

Mwanadiplomasia wa Marekani azuru Country FM

Na Mweha Msemo I Novemba 1, 2018 Ikiwa Country FM ni miongoni mwa wanufaika wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya Marekani hapa nchini, mmoja wa wanadiplomasia wa juu katika ubalozi wa nchi hiyo hapa Tanzania alifanya ziara ya siku moja katika kituo hiki ikiwa ni hatua za kufuatilia utekelezaji wa miradi husika. Chini ni.

Hali uwanja wa Nduli hairidhishi: RC Hapi

Na Philberta Kabonyela |Septemba 5, 2018 Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ally Hapi emeeleza kutoridhishwa na hali halisi ya uwanja wa ndege wa Nduli uliopo kata ya Nduli mkoani hapa katika kufanikisha maendeleo stahiki kwa manufaa ya wakazi wa mkoa wa Iringa. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati mdogo unaoendelea katika uwanja.

RC Hapi asimikwa uchifu wa Wahehe

Na Herieth Rebman | Agosti 11, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Salum Hapi leo amefanya mkutano na wazee wa Mkoa wa Iringa na kusimikwa rasmi kuwa Chifu wa kabila la Wahehe ikiwa ni ishara ya kumpokea na kumpa nguvu ya kuutawala mkoa huu. Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo,.

Mch. Msigwa amkaribisha Rais Magufuli Iringa, atoa tahadhari kwa wana-CHADEMA

Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa amewakaribisha wageni wote mkoani humo akiwemo Rais Magufuli katika kusherehekea siku ya Mei Mosi na kuwaomba wanachama wa CHADEMA na wafuasi wa UKAWA kutovaa sare za vyama kwenye sherehe hizo. Mchungaji Msigwa kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Mei 1, 2018 amesema kuwa viongozi wa Chama.

Country FM yanufaika uwezeshaji Internews, USAID

Na Herieth Rebman | Februari 22, 2019 Katika juhudi za kuboresha maudhui kwa vyombo vya habari vya Tanzania, shirika la Internews kupitia mradi wa USAID Boresha Habari wametoa vitendea kazi mbalmbali kwa radio jamii 19 huku Country FM ikiwa ni moja ya vituo vilivyonufaika. Zoezi la ugawaji vifaa lilifanyika Jijini Dar es salaam mara baada.